Micro Health Initiative - Mpango wa Afya Kilimanjaro

Lema Road, Shanty Town

Shanty Town, Moshi-Kilimanjaro

Toll Free

0800753326

FAQ’s

On this page we have collected the most important questions, so that you could easily find the answer for almost any question you have doubts to clarify.

Mpango wa Afya Kilimanjaro ni  mpango ulioandaliwa kukidhi mahitaji ya afya kwa wananchi wa kawaida wasio  katika makundi ya bima kama NHIF, NSSF nk

Mpango Wa Afya Kilimanjaro ni kwa ajili ya mtu yeyote ambaye anahitaji kuchangia kwa pamoja kupata matibabu . Zahanati, vituo vya afya, na hospitali  zitatoa huduma ya afya kwa mchangiaji.. Microhealth Initiative itasimamia huduma na kuratibu malipo kwa vituo vitakavyotoa huduma kwa wanachama watakaojiunga na mpango. Mpango huu  unafanikishwa na wadau kama vile, Microhealth Initiative, AAR (T), FSDT, SPRING na wengine

Mpango huu umepangiliwa kwa ngazi kadhaa kuu kuendana na uwezo wa kujiunga na mahitaji ya mwanachama, ngazi ya kwanza inajulikana kama “MAWENZI” inahusishisha matibabu ya Afya ya msingi ikiwemo kumwona daktari katika hospitali, kupata huduma ya maabara na dawa, Ngazi ya pili “KIBO” inahusisha matibabu yote ikiwemo kulazwa na ngazi ya mwisho “ AAR” ni matibabu ya juu kupitia AAR Tanzania na kutibiwa katika vituo vya AAR Tanzania nzima

Ndio, waweza pia kujiunga na Ngazi ya KIBO FAMILIA ambayo ni wewe na wategemezi wako watatu, wategemezi wako lazima wawe na umri mdogo kuliko wewe. Pia waweza kujiunga na Dadacard iwapo wewe in msichana wa miaka 10-24 au unaye mtoto wa umri huo

Waweza kujiunga ukiwa mahala popote Tanzania, ilimradi ukute bango la Jisajili Hapa – Micro Health Initiative .pia utapata huduama popote utakapokuta Micro Health Initiative huduma zinapatikana hapa.

MAWENZI CARD – 30,000, KIBOCARD Ni 60000, KIBO FAMILIA ni 160000, DADACARD ni 45000 na AAR ni 220,000

Huduma zinazotolewa na vituo vya matibabu kwa watakaojiunga na mpango huu ni zile ambazo zimeorodheshwa kwenye huduma makubaliano ya huduma kulingana na ngazi uliochagua. Kadhalika huduma za matibabu na kuzuia magonjwa sugu kama kisukari shinikizo la damu, na magojwa yanayotokana na kuwa na virusi vya ukimwi.

Ndio, dawa zote za magonjwa yanayotibiwa katika ngazi husika zitalipiwa na mfuko huu. Hutahitaji kuzinunua.

Ndiyo, vipimo vyote utakavyofanyiwa katika kituo ulichopangiwa vitalipiwa na mpango

Mtu yeyote anaweza kuugua siku yoyote. Hii inapotokea, Mpango wa afya unahakikisha matibabu ya hali ya juu yanapatikana kwa kuweka pamoja michango ya wanachama katika mfuko maalum na inatumia fedha hizi kulipia matibabu ya wale waliougua. Unaweza kuchangia mwaka ukaisha bila kuugua, lakini mwaka ujao inawezekana wewe ndiye unahitaji zaidi huduma hizi.

Hapana, kila mwanachama anawajibika kujiandikisha yeye na wategemezi wake wote ili kuhakikisha kuwa familia inapata matibabu kwa mlingano.

Hii itakuwezesha kuanza kupata huduma ya Mpango Wa Afya Kilimanjaro , na pia kuhakikisha kwamba orodha ya wanachama na familia zao imekamilika. Hii inazuia makosa au mapungufu madogo madogo wakati wanachama wanajiandikisha kwenye mpango huu, na pia itaweka tahadhari kwa watu ambao sio wanachama wanaotaka kutumia huduma isivyo halali au kinyume na taratibu.

Taarifa utakazozitoa zitatumika kwa ajili ya afya tu na zitahifadhiwa kwa siri. Taarifa hizi hazitatolewa kwa mtu mwingine yeyote zaidi ya washirika wa maendeleo wanaohusika katika mipango, utekelezaji na ufuatiliaji wa Mpango huu.

Utaweza tu kujiunga na Mpango muda wowote ndani ya mwezi husika.

Hakuna anayejua ni lini yeye au mmoja katika familia yake ataugua. Ni rahisi kujiunga na mfuko wa matibabu wa pamoja badala ya kulipia matibabu kutoka kwenye mfuko wako kila wewe au mmoja katika familia anapougua. Mpango huu unaboresha huduma katika vituo vya afya na zahanati kama:, kuwafundisha watoa huduma, kuhakikisha dawa zipo wakati wote, kutembelewa na madaktari bingwa, kuweka mifumo ya kumbukumbu ya computer, na pia jamii inashirikishwa kwenye maswala ya ubora wa huduma za afya ikiwemo huduma ya daktari kwa sms

Vituo vya matibabu vimechaguliwa katika maeneo ya karibu na makazi ya wanachama . Wahudumu wa afya wanapata mafunzoya ziada ili kuboresha utoaji wa huduma. Pia wataalam wa afya watafuatilia kuhakikisha huduma bora zinatolewa katika vituo vya matibabu kwa wakati wote.

IO. Vituo kadhaa vya matibabu vimechaguliwa ili kutoa huduma za afya kwa wanachama wa Mpango. Unawajibika kuchagua mojawapo ya kituo kama kituo chako cha kupata huduma. Hii ina maana kwamba unapougua au umejeruhiwa utaenda kutibiwa katika kituo cha matibabu ulichokichagua. Iwapo una dharura na unahitaji matibabu katika kituo ambacho hujachagua utatibiwa na utapewa fomu maaalum ya kutia sahihi kwamba ulipata dharura, pia ni lazima kituo hicho kiwe kwenye mtandao wa vituo

Vituo vya matibabu vilivyoteuliwa ni vile ambavyo vina wahudumu wote muhimu. Wahudumu wanapatiwa elimu na kujengewa uwezo zaidi ili waweze kutoa huduma kwa ufanisi. Wahudumu watakuwa wanafuatiliwa na wataalam wengine kuhakikisha huduma bora inatolewa katika vituo hivi vya matatibabu.

Unaweza kujiunga kupitia kwa kituo cha uandikishaji popote utakapoona bango la jiandikishe hapa la micro health initiative. Pia unaweza kupiga simu kituo cha huduma kwa wateja simu no. 0800753326 tukupe maelekezo ya ziada jinsi ya kujiunga

Kila mwanachama atakaejiandikisha atapewa kadi maalumu ya kumtambulisha kituoni pindi atakapougua.

Ongea nasi kupitia namba ya bure 0800753326 .Kwa taarifa zaidi pia unaweza Kufika ofisini kwetu Shanty town

Any Help Needed ?

Contact us for any questions or doubts on related to our product etc... drop us a mail and will get back to you as soon as possible with best solution.

Reach Us


Image

Sign Up for MHI Newsletter

 
Email